Wachezaji mashuhuri katika ligi
za soka za Uingereza na zile za Brazil wanajiunga na kampeni ya kuwaonya
mashabiki dhidi ya kuwatumia makahaba watoto wakati wa michuano ya
kombe la dunia nchini Brazil baadaye mwaka huu.
Wachezaji wa kilabu ya Chelsea Frank
Lampard,Oscar na Ramirez wanaunga mkono kampeni hiyo inayoshirikisha
kitengo cha kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza pamoja na serikali
ya Brazil.
Kampeni hiyo inawaonya wafuasi wa Uingereza
kwamba watakabiliwa na tisho la kushtakiwa iwapo watalipa ili kulala na
wasichana walio chini ya umri 18.
Taifa la Brazil linakadiriwa kuwa na nusu ya
milioni ya idadi makahaba watoto wanaosimamiwa na na magenge ya uhalifu
na kuna hofu kwamba idadi hiyo itaongezeka wakati wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment