Thursday, April 3, 2014

WANASIASA MAARUFU NA TIMU ZAO ZA SOKA


David Cameron


David Cameron ni Waziri mkuu wa Uingereza ni shabiki kubwa wa Aston Villa, aliiangalia mechi ya kwanza ya Aston Villa akiwa na umri wa miaka 13 tu alipochukuliwa na Sir William Dugdale  ambaye ni mjomba na pia ni mwenyekiti wa Aston Villa.

Silvio Berlusconi


Mwenyeji wa jiji la Milan ni shabiki mkubwa wa AC Milan ambayo mwaka 1986 ilikumbana na hatari ya kufilisika na hivyo akainunua ili kuinusuru timu hiyo na janga hilo.  Aliwekeza pesa za kutosha na kuiwezesha AC Milan kombe la Ulaya (ligi ya mabingwa ulaya) miaka mitatu baadae.

Francois Hollande


Fracois Hollande alizaliwa kaskazini mwa Ufaransa maeneo ya Rouen, ni mwanasiasa maarufu ambaye kwa sasa ndiye rais wa Ufaransa ni shabiki mkubwa wa AS Monaco. 

Prince Albert II of Monaco


Hautakiwi kujiuliza mara kumi kumi ni timu gani ya Ligi 1 Prince Albert wa pili anaishabikia. Ni shabiki mkubwa wa AS Monaco, wiki hii aliliambia gazeti Dello Sport la Ufaransa kamba angelipenda kumleta Ibrahimoc na baadae Mario Balotelli

George Galloway


Mwanasiasa mtata na makini ambaye ni mbunge wa Bradford Mashariki ni shabiki mkubwa wa Celtic

Vladimir Putin


Vladimir Putin rais wa Russia ni mwenyeji wa St. Petresburg ni shabiki mkubwa wa Zenit.

Barack Obama


Barack Obama alionesha umahili wake wa kuchezea mpira alipotembelewa Ikulu na klabu ya LA Galaxy mwaka 2013 ni shabiki mkubwa wa West Ham United ya nchini Uingereza. 

Mariano Rajoy


Marino Rajoy ni waziri mkuu wa Hispania, richa ya kuzaliwa na kukulia Galicia ni shabiki mkubwa wa Real Madrid.

Enrico Letta


Waziri mkuu na waziri wa kilimo  mstaafu wa Italy ni shabiki wa kutupwa wa Milani.

Gordon Brown


Waziri mkuu mstaafu wa Uingereza ambaye amekulia Kirkcaldy ambako Raith Rovers inapatikana. Ni shabiki mkubwa wa Raith Rovers na amewahi kuliambia gazeti la the guardian kwamba alianza kuwafuatilia akiwa na umri wa miaka 7 au 8 hivi.  Mwaka 2005 aliisaidia klabu hiyo kwa kununua hisa.

Cristina Kirchner


Ni raisi wa Argentina tangu mwaka 2007 ni shabiki mkubwa wa Club de Gimnasia y Esgrima La Plata ambayo inapatikana eneo alilozaliwa La Plata

Luiz Inacio Lula Da Silva


Luiz Inacio Lula Da Silva alikuwa rais wa Brazil, alihamia jiji la Sao Paulo akiwa mdogo na akakulia huko ambako akaanza kuipenda klabu ya Corinthians ambayo hadi sasa ndio klabu ambayo anaishabikia.

Nick Clegg


Naibu waziri mkuu alizaliwa na kukulia katika kijiji cha Buckingham, eneo ambalo mashabiki wa hali ya kati wa Arsenal wanapatikana. Ni shabiki mkubwa wa washika mtutu wa London Arsenal.

Ed Miliband


Kiongozi wa kambi ya upinzani ambaye inafahamika mapenzi yake makubwa ni katika mchezo wa baseball na American football lakini baadae akatangaza kuwa ni shabiki wa Leeds United.

Glenda Jackson


Glenda Jackson ameshinda tuzo mbili za Academy Awards kama muigizaji bora wa kike kwa sasa ni Mbunge wa Hamptsead na Kilburn ni shabiki mkubwa wa Tranmere Rovers.

Sebastian Coe


Mbunge kutoka Conservative ni shabiki mkubwa wa Chelsea

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...