Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa Shisha.Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye
ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa
mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana wadogo
mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha
wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili
wavitaji wa sigara.
No comments:
Post a Comment