Ufaransa ndiyo timu ya kwanza
kuwahi kufaidi matumizi ya teknolojia ya kisasa kuzuia ubishi katika
mechi ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil. Karim Benzema alikuwa anatekeleza mashambulizi
katika lango la Honduras kunaklo dakika ya 48 ya kipindi cha pili lakini
kipa wa Honduras Noel Valladares akababaika na mpira ukavuka laini
kisha akaunyofoa mara moja na kukimbia akitaka kuupiga kama 'goal
kick' lakini mpiga kipenga kutoka Brazil Sandro Meira Ricci akapuliza
kipenga na kuashiria bao kutokana na mtikiso kwenye saa yake
inayoambatana na teknolojia hiyo ya kisasa ya goal line.
Mashabiki na wachezaji wa Honduras waliokuwa
ndani ya uwanja wa Porto Alegre walijaribu kupinga kauli ya refarii huyo
lakini wapi alihakiki bao hilo la pili usiku huu kwa Ufaransa .
Honduras ilikuwa tayari imempoteza mchezaji wao Palacios mwisho wa kipindi cha kwanza alipoonyeshwa kadi ya pili ya manjano
Teknolojia hiyo inayotumika kwa mara ya kwanza
inajumuisha kamera 14 za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa kurekodi picha
na sauti kwa kasi mno na mpira ambao inasambaza
Kamera hizo zinauwezo wa kuchukua picha kwa kasi mno (saba kwenye kila lango), katika paa za nyanja zote 12, Brazili. Kamera hizi zimeunganishwa kwenye tarakilishi
inayounda maumbo na kuondoa umbo lolote lile ambalo sio la mpira, kisha
kufuata mwenendo wa mpira kwa kadri milimita chache, kampuni hiyo
ilisema. Mpira unapovuka tu mstari wa lango, utakuwa
unapeperusha ujumbe kwenye saa yake mwamuzi wa mechi, kisha ujumbe wenye
maandishi ‘GOAL’ unatokea kwenye saa hiyo pamoja na mtikisiko
(Vibration). Haya yote yanafanyika kwa muda wa chini ya sekunde moja.
Mfumo huo ambao tayari ushajaribiwa na Fifa, katika kombe la Mashirika mwaka uliopita.
Kampuni ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa
kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa,
ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya michezo.
Hii itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la
dunia kuonyeshwa katika mfumo wa kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High
Definition (UHD), ujulikanao kama 4K Format, ambayo kiwango chake ni
mara nne zaidi ya kiwango cha televisheni za kawaida.
Hata ingawa suluhisho hii imetumiwa kwa miaka
mingi katika michezo mingine,kama Tennis Cricketi na Raga hii itakua
mara ya kwanza teknolojia ya lango la goli kutumika katika kombe la
dunia .
Ni mfano mmoja tu wa jinsi kombe hili la dunia
litakavyokua lenye teknolojia kubwa zaidi na lenye kujumuisha miundo
mbinu ya teknolojia ya karne ya 21.
No comments:
Post a Comment