Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba bondia anayewakilisha vyema mkoa wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela miaka 3. Chanzo cha habari kinatujuza kwamba Cheka amehukumiwa miaka 3 kwa kosa la kumpiga mfanyakazi wake ambaye alikuwa anamfanyia biashara ya kuuzwa vinywaji. Baada ya muda Mfanyakazi huyo akaanza kumkimbia Cheka ambaye naye alikuwa anatamtafuta, baadae akafanikiwa kumpata na kutembezea kichapo kilichomfanya kwenda kuripoti polisi na baadae kesi kupelekwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment