Showing posts with label entertainment. Show all posts
Showing posts with label entertainment. Show all posts

Saturday, March 15, 2014

Kigwema aachia ngoma mpya


Msanii Kigwema Bosco maarufu kama Kigwema ameachia ngoma kali inayokwenda kwa jina la Narudi Nyumbani. Kigwema ambaye ni maarufu kwa  ubunifu wa mawazo tofauti tofauti kwenye track zake kama vile binti skendo na sitomsahau, kwenye track hiyo amemshirikisha Crush B. Nyumbani ina maana nyingi, inawekuwa pale unapoishi yaani nyumba, mtaa, wilaya, mkoa au nchi. Je, unataka kujua Kigwema anarudi wapi?
download track hiyo kwenye hii link upate burudani 

KIGWEMA ft CRUSH B - NARUDI NYUMBANI

Friday, March 14, 2014

M Rap aachia ngoma mpya

Msanii M Rap alieamua kuondoka BHits baada ya mkataba wake kukamilika, ameachia wimbo mpya "Usiende Mbali" akiwa na Jux kupitia studio za AM na producer Bob Manecky.
Baada ya Pancho na Mwanasheria wake kuja Bills juma pili iliyopita (9 March) na kumzuia ku-perfom nyimbo ambazo amezirecord akiwa chini ya lebo hiyo baada ya kuamua kuondoka katika lebo hiyo, M Rap aliamua kuingia studio na kukesha usiku mzima kurecord mpaka kukamilisha single ya kwanza chini ya studio za AM.
 
"Nilikuwa na hasira sana na stress ndio maana niliamua kuingia studio na kutengeneza wimbo huu nikiwa na jux"
 
 

Thursday, September 12, 2013

PEEN LAWYER AOMBA SUPPORT KWA MASHABIKI WAKE


Msanii wa kizazi kipya Peenlawyer amewaomba mashabiki wake mawazo kuhusu video ya wimbo wake mpya  HARAKATI (MOVEMENT) ambao unaelezea siasa za bongo. Tatizo kubwa ni kwamba yeye yupo nchini Ujerumani na anahitaji kufanya video ya hiyo ngoma ambayo inahitaji kuwa na location za hapa Tanzania kwa sababu inaongelea siasa ya bongo. Kwa hiyo anahitaji mawazo kutoka kwa wadau wa muziki wake aifanye kwa mtindo upi hii video. Akisistiza hilo Peenlawyer ameandika yafuatayo katika ukurasa wake wa facebook.

NIMEKUMBANA NA TATIZO AMBALO NAHITAJI MSAADA WA MAONI YENU NDUGU ZANGU nataka kufanya video yangu hii HARAKATI,,now tatizo nikuwa Nyimbo inaongelea siasa za Tanzania na mimi nipo Ujerumani,,sasa ukiwa umeisikiliza hii ngoma plz naomba maoni ya ya hii video japo kwa mstari mmoja mmoja wowote wa verse yeyote...! niambie nifanye kwa style ipi..! au tuipotezee tufanye video nyingine? ushauri plzzz..... ntatumia idea zunu....!

UKITAKA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD COPY LINK HIYO CHINI THEN SEARCH

  http://www.reverbnation.com/play_now/song_18462041
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...