Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria
mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu
uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi
sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha
kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama
hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa
michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala,
waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa
Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili
bada ya bunge kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya
vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha
kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote
atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu
uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu
walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia
visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya
kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Maandamano ya kupinga agizo la wanawake kutovalia sketi fupi
No comments:
Post a Comment