Simba
ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo
imepigwa faini ya sh. 500,000. Pia imepigwa faini nyingine ya sh.
500,000 kwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia
uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.
Naye
mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa
kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya
matusi kwa kidole.
Mbeya
City imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia uwanjani
kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba. Klabu za
Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa
washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo
zilipopambana jijini Tanga.
Kiungo
wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa
kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar
amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya
Mbeya City.
Pia
mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000
kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo
vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh.
500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.
Nayo
JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani
kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Vilevile
wamiliki wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wameandikiwa barua ya
kufanya marekebisho ya vyumba vya wachezaji, kwa vile havina hewa ya
kutosha.
Kwa
upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) klabu zilizopigwa faini kutokana
na makosa mbalimbali ni Friends Rangers (sh. 200,000), Lipuli (sh.
200,000), Majimaji (sh. 400,000), Polisi Morogoro (sh. 400,000) na
Transit Camp (sh. 200,000).
Kocha
Msaidizi wa Polisi Morogoro, John Tamba atapelekwa kwenye Kamati ya
Maadili kutokana na vitendo visivyo vya kimaadili katika mechi dhidi ya
Burkina Faso.
Kiongozi
wa Lipuli, Hamis Kiemba na wachezaji Boniface Sawaka, George Enock na
Green Paul watapelekwa katika Kamati ya Nidhamu kutokana na utovu wa
nidhamu waliofanya kwenye mechi dhidi ya Kimondo.
Naye
mchezaji Sangalau Nyamoka wa JKT Kanembwa aliyelalamikiwa uhalali wake
na Polisi Tabora suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu.
No comments:
Post a Comment