Friday, March 7, 2014

Wimbo wa Nash MC umesababisha kituo cha radio kupewa onyo kwa madai ya kuwa na maudhui ya uchochezi




Mamlaka ya Mawasiliano nchini -TCRA- imekipa onyo kituo  cha  utangazaji cha  Radio Free Afrika kutokana na kupiga muziki  wa rapper wa Tamaduni music, Nash Mc kwa madai kuwa wimbo huo ni mahudhui ya uchochezi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa mamlaka hiyo Magreth Mnyagi amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa hukumu juu ya  kosa hilo.
Amesema kosa hilo ni la ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005 hivyo kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kushauriana na kamati ya maudhui ya vipindi vya radio kutoka TCRA.
Bi Magreth amesema wimbo huo ulichezwa June mwaka jana. Kwa kuzingatia kauli hiyo inawezekana wimbo ni ‘Kaka Suma’, wimbo uliokuwa unazungumzia kupanda kwa nauli za daladala.

Credits kwa timesfm.co.tz

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...