Muimbaji na muigizaji wa filamu nchini,
Hemedy PHD amesema anaamini amefanikiwa kuziba pengo la marehemu Sharo
Milionea aliyeigiza kwenye filamu kadhaa kama mtoto wa muigizaji
mkongwe, King Majuto.
Hadi sasa Hemedy ameshaigiza zaidi ya filamu tatu za komedi na
Majuto na amesema wametokea kupatana mno kiasi cha kufanya filamu
wanazoigiza pamoja zivutie kama zilivyokuwa filamu za Sharo Milionea na
Majuto.
Hemedy amesema Majuto ameamuamini Hemedy kiasi cha kumwambia kuwa
anaweza kuandaa filamu yake mwenyewe ambayo atashiriki kwa mikono yake
miwili.
“Kwahiyo itakuwa ni kazi ambayo ipo kibaba na kimwana zaidi kuliko
kibiashara zaidi which means ni mzee ambaye anakubali ninachofanya na
anaappreaciate sana,” ameongeza.
Kwa sasa Hemedy na King Majuto wapo jijini Mwanza kushoot filamu yao mpya ya komedi iitwayo Kimbulu.
No comments:
Post a Comment