Wananchi ambao wanatumia daraja linalounganisha Bunju B(Dar Es Salaam) na kijiji cha Mapinga (Bagamoyo) wamejikuta wakitumia njia mbadala ya kuvuka baada kukatika kwa mawasiliano baina ya pande hizo mbili. Baadhi ya vijana wa eneo hilo wamebuni usafiri mbadala kwa kuwavusha watu na mizigo kwa kuwabeba au kuwashika mkono ilikuvuka mto huo ambao una maji mengi ambayo yanatiririka kwa kasi. Vijana hao wanavusha mtu mmoja kwa shilingi 1,000/= na mzigo kwa shilingi 2,000/= mpaka 3,000/=
Dada ambaye jina lake halikupatikana akivushwa kuelekea upande wa Bunju (Dar Es Salaam)
Vijana wakipokea wateja wa kuwavusha ili kujipatia kipato.
Wengine walikuwa wanavushwa kwa kushikwa mkono.
Sio watu tu hata mizigo nayo ilikuwa inavushwa kwa kiasi cha shilingi 2,000/= hadi 3,000/= pesa halali za kitanzania kwa mzigo.
No comments:
Post a Comment