Mwanamke anayeshikilia cheo cha
juu zaidi katika kampuni ya Facebook, amewataka wanawake kuchukua hatua
za kubuni mazingira ya usawa kote duniani.
Sheryl Sandberg, afisaa mkuu wa mipango katika
Facebook, amesema kuwa wanawake, wanapaswa kushikilia nafasi muhimu
katika biashara.
"ikiwa unatafakari kuhusu kufanya
kitu, jiulize nini unachoweza kufanya ikiwa hauna uoga na basi
ukifanye,'' Bi Sheryl aliambia BBC.
Sandberg ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika kampuni hiyo tangu mwaka 2012.
Mwaka jana aliandika kitabu kwa jina 'Lean In'
ambacho kinawashauri wanawake kuhusu wanavyoweza kupiga hatua katika
nafasi zao za kazi.
"ni muhimu sana kwamba wanawake ambao ni nusu ya
idadi ya watu wote, waanze kushikilia vyeo katika meza za maamuzi ,
lakini bado hatujafika hapo, '' alisema .
Alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi muhimu sana katika biashara,serikali ni pamoja na kuwa wajasiri amali
Akizungumzia baadhi ya changamoto zinazokumba
Facebook, Sandberg alisema kuwa dunia inashuhudia mageuzi makubwa ya
kiteknolojia ambayo yanahusisha simu ya rununu na Facebook ipo katikati
ya mageuzi hayo
No comments:
Post a Comment