Dar es Salaam. Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi amejibu baadhi ya hoja za watu wanaopendekeza muundo wa serikali mbili na kusema Serikali ya Zanzibar ndiyo iliyoanza kutaka serikali tatu mwaka 1984.”
Aidha, amewashangaa wanaolibeza jina la Tanganyika
kutumika serikalini kwa madai kuwa jina hilo siyo haramu kwa kuwa limo
ndani ya Katiba ya sasa.
Alisema kuwa wakati huo madai ya serikali tatu yalitolewa na Zanzibar na kusimamiwa na Rais aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaji Aboud Jumbe.
“Hoja ilipelekwa pia kwenye Baraza la Wawakilishi,
Brigedia Mstaafu Ramadhan Haji Fakhi (aliyekuwa Waziri Kiongozi),
alikuwa akiongea kwa sauti nzito, kama ulikuwa ukimsikiliza, unasema
muungano haupo,” alisema Profesa Kabudi na kueleza kuwa Fakhi alisema:
“Zanzibar siyo koloni la Tanganyika.”
Alikuwa akichangia hotuba katika Kongamano la Kujadili Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika mjini Zanzibar jana. Alieleza kwamba mjadala wa sasa wa muungano siyo mkali kama uliokuwepo mwaka 1983 na 1984.
Hata hivyo, hotuba hiyo ya Profesa Kabudi iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) ilikatishwa kabla mzungumzaji kumaliza hotuba yake.
Katika maelezo yake, Profesa Kabudi ambaye pia ni
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kuwa Fakhi alikuwa
haongei kama mtu baki, bali aliagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“Lugha ilikuwa ni kali,” alisema.
Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal alisema kuwa
masuala mengi yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanaibuliwa na wanasiasa.
“Unawezekana kuwa muungano unatunyima fursa moja
ua mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini
wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa
zao, lakini wahakikishe wanawahudumia wananchi,” alisema.
Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo siku chache baada ya
Rais Jakaya Kikwete na baadhi wanasiasa kutoka CCM, wakiwamo Wajumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba kuikosoa Rasimu ya Katiba Mpya.
Kikwete pamoja na wajumbe hao kwa nyakati tofauti,
walisema kuwa Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba haionyeshi uhalisia wa matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu
muundo wa muungano.
“Unaweza kuwa muungano unatunyima fursa moja au mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao lakini wanahakikisha wanawahudumia wananchi,” alisema.
Akifafanua matumizi ya jina la Tanganyika kwenye Katiba ya sasa, Profesa Kabudi alisema: “Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya nne, 34, 64, 102 na 151, inaonyesha kuwa zipo mamlaka tatu. Mamlaka ya masuala ya muungano na mamlaka ya masuala yasiyo ya muungano katika upande wa Tanzania Bara (Tanganyika).”
Alibainisha: “Nataka niwaambie, leo ukienda kwenye Ibara ya 151 ya Katiba, Tanzania Bara imetajwa kuwa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, kwa hiyo hata Katiba ya sasa Tanganyika ipo, kwa hiyo Tanganyika siyo jina haramu.”
Hati ya Muungano
“Hili suala la kwamba hati zipo au hazipo siyo suala kubwa, suala ziliridhiwa? Ushahidi upo upande wa Tanganyika ziliridhiwa. Kwa upande wa Zanzibar kuna utata na hiyo kesi ipo mahakamani,” alisema.
Alisema kutokana na utata huo katika Rasimu, wakapendekeza namna ya kutatua tatizo lililodumu kwa miaka 50 kwa kuandika kuwa hati ya maridhiano ya Tanganyika na Zanzibar kuwa msingi mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akifungua kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal, alisema kuwa masuala mengi
yanayoleta mgogoro kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanaibuliwa
na wanasiasa.
“Unaweza kuwa muungano unatunyima fursa moja au mbili, unatunyima uwezo wa kuamua katika masuala hayo, lakini wananchi hawayaoni hayo. Muungano ni wa wananchi, viongozi wana fursa zao lakini wanahakikisha wanawahudumia wananchi,” alisema.
Akifafanua matumizi ya jina la Tanganyika kwenye Katiba ya sasa, Profesa Kabudi alisema: “Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya nne, 34, 64, 102 na 151, inaonyesha kuwa zipo mamlaka tatu. Mamlaka ya masuala ya muungano na mamlaka ya masuala yasiyo ya muungano katika upande wa Tanzania Bara (Tanganyika).”
Alibainisha: “Nataka niwaambie, leo ukienda kwenye Ibara ya 151 ya Katiba, Tanzania Bara imetajwa kuwa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, kwa hiyo hata Katiba ya sasa Tanganyika ipo, kwa hiyo Tanganyika siyo jina haramu.”
Alisema anaamini kila taifa lina ujinga wake
katika kutunga Katiba, lakini ujinga wa kizazi kimoja hauwezi kuwa wa
kizazi kingine.
“Ujinga wa kizazi hiki, tusidhani utakuwa ujinga wa kizazi cha kesho, vizazi vijavyo vya Tanzania vitakuwa na ujinga wake.”
Alifafanua: “Ni vyema kuwawekea misingi lakini
waje kuishi na ujinga wao, kuliko kulazimisha ujinga wako, kwa sababu
wewe ujinga wako ndiyo amali yako lakini kwa wengine siyo amali.
Ulitegemea Waingereza wangekapigia mizinga kachanga ka siku moja?”
Hati ya Muungano
Akizungumzia hati ya muungano iliyozua sintofahamu
hivi karibuni kwa madai kwamba haikuwepo, alisema msingi wa kikatiba na
kisheria wa muungano wowote ni hati za muungano.
Alisema miaka ya 1980, suala lililokuwa
linajadiliwa ni iwapo hati za muungano ni sehemu ya sheria za kimataifa
au la. Baadaye ilibainika kuwa hati hizo ni mkataba wa kimataifa na
kwamba unatawaliwa na sheria za kimataifa.
“Hili suala la kwamba hati zipo au hazipo siyo suala kubwa, suala ziliridhiwa? Ushahidi upo upande wa Tanganyika ziliridhiwa. Kwa upande wa Zanzibar kuna utata na hiyo kesi ipo mahakamani,” alisema.
Alisema kutokana na utata huo katika Rasimu, wakapendekeza namna ya kutatua tatizo lililodumu kwa miaka 50 kwa kuandika kuwa hati ya maridhiano ya Tanganyika na Zanzibar kuwa msingi mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment