TAMKO LA KKKT KUHUSU KATIBA MPYA
Msaidizi
wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kikristo Tanzania (KKKT), Dayosisi
ya Dodoma Mchungaji Samweli Mshana, amewataka wajumbe walio katika
mchakato wa Katiba kuhakikisha wanawapatia watanzania Katiba itakayotoa
haki zote bila upendeleo.
Aidha, alisema kanisa hilo halitarajii Katiba hiyo kumilikiwa na vyama vya siasa na viongozi wao au kuwa ya kiitikadi.
Mchungaji Mshana alisema hayo akizungumza katika tamasha la akinamama KKKT Jimbo la Makao Makuu, Dodoma.
Mchungaji huyo alisema hatarajii kuona wajumbe hao wakijadili Katiba kwa kupendelea upande wowote ule wa jamii.
Naye
Mwenyekiti wa Wanawake Jimbo la Makao Makuu KKKT Dodoma, Salome Kingu
alisema wanawake wa jimbo hilo tangu lianze Bunge hilo la Katiba
wamekuwa wakimlilia Mungu ili Katiba iweze kuwa ya Watanzania wote na
itakayojali haki.
Katika
tamasha hilo mafundisho mbalimbali yatafundishwa ikiwemo somo la
Maadili ya Mwanamke katika kanisa na Ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia
kwa wakati huu tulionao na somo la Maadili ya Wanawake, Sheria na
Mirathi.
No comments:
Post a Comment