Mwenyekiti
wa Yanga SC, Yussuf Manji (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari Jana
Agosti 29,2014. Kushoto Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga.
Klabu ya
Yanga imekana kumpa barua Emmanuel Okwi ya kuvunja naye Mkataba na imesema
mshambuliaji huyo Mganda, amewahadaa Simba SC ambao wameingia mkenge wakati
akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga.
Yanga SC imeandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiiomba ifanye
mambo mawili- 1- imfungie Okwi kucheza soka na 2- iifungie Simba SC.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa jana Agosti
29,2014, makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar
es Salaam, Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amesema kwamba anaipa TFF siku
saba kutekeleza hayo.
Manji
amesema, iwapo TFF itashindwa kutekeleza hayo ndani ya siku hizo saba, wao
watahamia Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambako kama hawatafanikiwa
pia, watahamia Mahama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).
Manji amesema asubuhi wametuma malalamiko yao kimaandishi TFF na pia wanamdai
Okwi fidia ya dola za Kimarekani 500,000 (Sh. Milioni 900) kutokana na kuvunja
mkataba na wao.
Mwenyekiti
huyo amesema kwamba, kabla ya jana katika malalamiko ya awali waliyotuma TFF,
walitaka Okwi awalipe dola 200,000 (zaidi ya Sh. Milioni 340,000), lakini baada
ya Simba kutangaza imemsajili Agosti 28,2014, dau limepanda.
Manji amesema kwamba Yanga haina ubaya na Simba, bali watani wao hao wa jadi,
wamefanya vibaya kumsainisha mchezaji huyo bila kuwasiliana nao.
|
No comments:
Post a Comment