Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuchukua watu 60,0000
Serikali imekataa ombi la chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuutumia uwanja wa Taifa kwa shughuli ya uzinduzi wa kampeni zinazotarijiwa kuanza tarehe 22 mwezi huu wa nane, ikisema mazingira ya sasa hayaruhusu kufanyika kwa shughuli za kisiasa katika uwanja huo na hakuna chama chochote ambacho kitaruhusiwa kufanya hivyo. Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Habari Maelezo bwana Assah Mwambene amesema Serikali haijatoa ruhusa kwa chama chchote cha siasa kufanya shughuli za kisiasa katika uwanja huo.
No comments:
Post a Comment