Aliyekuwa naibu katibu mkuu bara, Julius Mtatiro amepitishwa
kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kupitia chama cha Cuf chini ya mwamvuli
wa UKAWA. Kupitia ukurasa wake wa facebook Mtatiro ameandika ‘‘ Leo chama change
kimenipa ridhaa na barua rasmi ili nigombee ubunge kwa tiketi ya Ukawa,
nimetoka kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Segerea”.
“Natumaini kuwa tutaanza kwa nguvu na kumaliza kwa ushindi. Nawaahidi
nitaunganisha vyama vya CUF, Chadema, NCCR na NLD kushirikiana na wananchi wa
Segere kupata madiwani wa kata zote 13’’
No comments:
Post a Comment