Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi (SACP) Ulrich Mtei
Marehemu Joseph Ngonyani
*************
Mnamo 11/06/14 majira ya 0100hrs
huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa
ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kiman nanzi Chana huku
wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni
watu wanaohitaji msaada. Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye
silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata
mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza
kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na
risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka
kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu
kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE
amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu
wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana
na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu
wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki
akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili
kwa matibabu ya kina. Pia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Taarifa kamili itatolewa.
No comments:
Post a Comment