
Mwanamume raia wa Kenya anayeshabikia klabu ya soka 
ya Uingereza ya Liverpool amedungwa kisu na mwenzake wa klabu ya Arsenal
 na kufariki dunia katika eneo la Meru Mashariki mwa Kenya.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo wawili hao walianza malumbano baada ya mechi kati ya vilabu hivyo kumalizika hapo Jumamosi.
Wawili hao walikua katika baa moja iliyojaa mashabiki wa timu hizo mbili.
Shabiki wa Arsenal anayefanya kazi ya Boda Boda 
alijawa na hasira baada ya timu yake kukemewa na shabiki wa Liverpool 
kiasi cha kumdunga mwenzake kisu mara kadhaa, kabla ya kutoweka.
Watu waliokua karibu na eneo la tukio hilo 
walimsaidia mwathiriwa aliyetambuliwa kama Anthony Muteithia na 
kumpeleka katika hospitali kuu ya Meru ambapo alifariki dunia wakati 
akipokea matibabu.
Mkuu wa polisi eneo la Meru Tom Odero amesema wanamsaka shabiki huyo wa Arsenal ambaye amekwenda mafichoni.
Hapo Disemba mwaka jana shabiki wa klabu ya 
Manchester United nchini Kenya kwa jina Jimmy Macharia alijiua baada ya 
klabu hiyo kuendelea kuorodhesha matokeo mabaya.
Na mnamo mwaka 2012 Suleiman Alfonso Omondi 
shabiki wa Arsenal alijitia kitanzi baada ya timu hiyo kushindwa kwenye 
mechi. Ligi ya Premia nchini Uingereza huvutia ushabiki mkubwa nchini 
Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment