Wednesday, March 26, 2014

KIGWEMA KUSHOOT NGOMA YAKE KWA KUSHIRIKIANA NA MASHABIKI WAKE


 
Kuna wasanii wachache sana ambao huwa  wanaproud  maeneo wanayotoka kama vile Weusi toka A City, Izzo B toka Mbeya City, Fid Q toka Mwanza na wengine kibao. Ukiongelea maeneo ya kusini mwa Tanzania, kuna miji ya Lindi ama Paris na Mtwara ama Gas City na Ruvuma kuna kichwa cha muziki ambacho miaka kadhaa iliyopita alichukua tuzo ya mwanamziki bora chipukizi kwenye tuzo za kili, na huyo si mwingine ni Kigwema Bosco hit maker wa ngoma kama binti skendo, sintomsahau na kwenye magazeti.

Mkali huyo hivi karibuni aliachia ngoma inayokwenda kwa jina la Narudi Nyumbani akimshirikisha mkali mwingine kutoka pande Crush B. Katika ngoma hiyo Kigwema kafunguka mengi sana kuhusu Nyumbani ambako anarudi kwa maana nyingine ni kusini.

Ili kuonesha msisitizo Kigwema anatarajia kufanya video ya wimbo huo maeneo ya kusini mwa Tanzania kuanzia Somanga mpaka Mtwara kuanzia siku ya jumamosi. Pia Kigwema ametoa Tshirt bomba ambazo zimeandikwa NARUDI KUSINI ili zivaliwe wakati wa kushoot pia unaweza ukanunu kwa matumizi mengine kwa ajili ya kung'aa mitaani. Kwa hiyo ukiwa kama mdau unaweza kumpa sapoti Kigwema ili aweze kufanikisha project zake salama.

kwa maelezo zaidi kuhusu unazipataje Tshirt na jinsi ya kushiriki kwenye hiyo video soma alichokiandika kwenye ukurasa wake wa facebook

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...