Wasamalia wema wakifunuka mwili marehemu baada ya kutoka kwenye jeneza.
Gari lilipata ajali likiwa limevamia nyumba lakini halikuweza kuleta madhara yeyote kwenye nyumba hiyo.
Ajali ya kusikitisha imetokea maeneo ya Bunju B karibu na
darajani leo majira ya saa 5 asubuhi, ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya
Defender lenye namba T289 CJX ambalo lilikuwa linasafirisha mwili wa marehemu kutoka Dar kwenda
Bagamoyo kwa ajili ya maziko.
Chanzo cha ajali hiyo ni kwamba dereva wa gari ambalo lilikuwa limebeba maiti alikuwa anaovertake gari nyingine, ambapo ghafla alilikutana na lori , baada ya kuona hivyo dereva ilimbidi achepuke barabara kuu na kuingia kwenye korongo na kufanya gari hilo kupinduka mara tatu na kuvamia nyumba.
Shuhuda na mpiga picha wa blog hii Yassin Walley anatujulisha kwamba mpaka sasa hakuna mtu yeyote ambaye
amepoteza maisha ila kuna baadhi ya majeruhi ambao wako taabani
akiwemo mume wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kupatikana maramoja.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo
mmmmmm kwa hiyo marehemu kafa mara mbili???????.....
ReplyDeleteDuuh! Maswali engine?
ReplyDeletePolebi sn
ReplyDeleteDu poleni sn...
ReplyDeleteJamani hii ajali huyu alolala chini ni shemeji wa marehemu sio mume wake na cha kusikitisha ni kuwa alifariki baada ya muda mfupi. Kibaya zaidi baada ya mazishi yake huko mbinga mkewe naye amefariki juzi uck wa kuamkia jumapili kwa BP! Bwana ametoa na bwana ametwaa....
ReplyDeleteTaswirabongo asanteni kwa taarifa
Thanks and that i have a super offer you: Who Repairs House Foundations local remodeling companies
ReplyDelete