Uingereza wametoa jezi mpya za nyumbani na ugenini
ambazo watatumia kwenye kombe la dunia mnamo mwezi 6 mwaka huu huko Brazil. Jezi
hizo zimetengenezwa na kampuni ya Nike, ambapo Uingereza watatumia jezi zenye
rangi nyeupe kama za nyumbani na nyekundu kama za ugenini. Jezi hizo zitaanza
kuuzwa tarehe 3 mwezi wa nne.
Kwa upande mwingine, wadadisi hasa wapenzi na mashabiki
wa Uingereza wanajiuliza hawa wachezaji Ross Barkley, Raheem Sterling na Alex Oxlade
Chamberlain, Gerald, Hart, Wilshere na Sturridge
ambao wametumika kwenye hizi picha za kutangaza jezi, Je ndio tayari wamepata
tiketi ya kwenda kule Brazil? Utata unakuja zaidi kwa mcheaji wa Everton
Barkley ambaye kabla alionekana ni 50/50 kuitwa kwenye kikosi au kuachwa. Tusubiri tuone.
No comments:
Post a Comment