Sunday, March 30, 2014

MAMBO KUMI (10) USIYOYAJUA KUHUSU CHRISTIAN BENTEKE



1 \1.Familia yake ilikimbia nchi ya Congo DRC
Christian Benteke alizaliwa Kinshasa, mji mkuu wa DRC. Familia yake ilikimbia nchi kuogopa utawala wa kidkteta wa Mobutu Sese Seko. Walihamia Liege, Ubelgiji. Alikuwa na miaka mitatu pindi wanahamia Ubelgiji.

     2. Jina lake la mwisho ni Liolo
Japokuwa watu wanamfahamu kama Christian Benteke, jina lake kamili ni Christian Benteke Liolo. 

3.Amechezea vilabu vitatu vya utotoni
Utotoni amechezea vilabu vitatu ambavyo ni JS Pierreuse aliyojiunganayo akiwa na umri wa miaka 6 mpaka mwaka 2004, Standard Liege (2004-2006) na Koninklijke Racing Club Genk (2006-2007).

4. Ni staa wa soka tangu utotoni
Utotoni alichezea vilabu vya  Standard Liege (2004-2006) na Koninklijke Racing Club Genk (2006-2007 ambako alijulikana sana kwa upachikaji wake wa mabao. Aliisaidia Standard Liege kushinda ubingwa wa ligi daraja la kwanza mwaka 2009.

5. Ni mtu wa imani
Kila akifunga goli Benteke huwa anaangalia juu na kuonesha vidole vyake juu. Kwa maelezo yake mwenyewe hiyo ni ishara ya kumshukuru Mungu.

          6. Amecheza michezo zaidi ya 60 tangu ajiunge na Aston Villa
Benteke amecheza michizo za ya 60 tangu alipojiunga na Aston Villa 2012 mwezi wa nane (8)

     7. Benteke ana wastani mzuri wa kufunga
Christian Benteke ana wastani mzuri wa kufumania nyavu kwa kila mechi ambao ni 1.939

8. Amechezea klabu kadhaa kabla ya kutua Aston Villa
Christian Benteke kabla ya kutua Aston Villa alichezea vilabu kadhaa, ukiaachana na vile ambavyo alichezea utotoni pia amechezea vilabu vya  KV Kortrijk (2009-2010) na Mechelen (2010-2011).
 

     9. Amepata kadi 11 tu
Tangu aanze soka la professional Benteke amepata kadi 11 tu, ambazo katika hizo kaoneshwa kadi nyekundu  1 tu na 10 za njano.

     10. Benteke huwa anatuma pesa nyumbani lakini hajawahi kurudi
Ingawa huwa anasema anahitaji kurudi mahali alipozaliwa siku moja. Benteke anaamini kwamba hali ya usalama kwa DRC bado haimshawishi kutembelea. Benteke anamatumaini ya kutembelea ardhi ya nyumbani siku za mbele. Lakini katika moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya alinukuliwa akisema kwamba huwa anatuma pesa kwa ndugu na jamaa za waliopo DRC ili ziwasaidie.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...