Wednesday, March 26, 2014

SHAKIRA AACHIA WIMBO KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA



Mkali wa Pop kutoka Columbia ameachia ngoma mpya kwa ajili ya kombe la dunia mwaka 2014 litakalofanyika mwezi wa sita mwaka huu huko Brazil. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye ni mpenzi wa mchezaji wa Barcelona Gerald Pique mwaka 2010 alitoa ngoma ya Waka Waka baada FIFA kumuomba kufanya hivyo na kumlipa, lakini mwaka imekuwa ni tofauti kwa Shakira hajaombwa na FIFA kuandika wimbo kwa ajili ya kombe la dunia, badala,ila Shakira yeye amefanya hivyo kwa matakwa yake mwenyewe.
Ngoma hiyo inaitwa "La La La" inategemewa kufanya vizuri kwenye vyombo vya habari mbalimbali hapa duniani, ikumbukwe pia wimbo wa Waka Waka ambao aliutoa mwaka 2010 unaungoza kwa mauzo kwa nyimbo za kombe la dunia za muda wote pia ukashika namba nane katika listi ya video ambazo zimeangaliwa sana Youtube

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...