Mtayarishaji wa muziki wa kizazi hapa Bongo Sheddy Clever A.K.A Mr Keyboard kupitia ukurasa wake wa facebook amefunguka na kusema kuwa wimbo wa Number One wa Diomond ndio wimbo ambao alichukua muda mwingi sana kuliko ngoma zote ambazo amewahi kutayarisha. Sheddy anasema kabla ya Number One alikaa kimya kwa muda mrefu kama wa miezi sita hivi bila hit yeyote ile hewani mpaka alipokutana na Diamond na kufanya Number One.
Sheddy hakujua kwamba kitu kizuri hakitaki haraka kiasi cha kuona kama anapoteza sana muda wake kwa kupika track hiyo, kwani ilifika hatua anatumia siku nzima studio na Diamond kushughulikia verse moja tu, lakini baada ya ngoma kuwa tayari na kwenda hewani na kupokelewa vizuri na wadau wa mziki sasa anaamini mambo mazuri hayataki haraka.
Sheddy anasema ngoma hiyo imemletea mafanikio makubwa sana, imemfanya akutane na watu wengi sana ndani na nje ya nchi. Pia sheddy ambaye anawania tuzo ya KTMA katika kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya wa mwaka anawashukuru sana mashabiki kwa sapoti ambayo wanaitoa kwa kazi zake
.
No comments:
Post a Comment