Imeandaliwa na Nurdini Mohamedi kwa msaada wa mitandao
Golikipa: Manuel Almunia
Ni golikipa ambaye alikuwa haeleweki kiwango chake, baadhi ya mechi anacheza vizuri lakini nyingine ni majanga, alikuwa na makosa mengi. Alirithi milingoti mitatu kutoka kwa Jens Lehman ambaye alikuwa katika kiwango cha hali ya juu lakini tofauti na matarajio ya wengi kiwango chake hakikuwa cha kuridhidhisha kulinganisha na makipa wengine ambao Wenger amewahi kuwasajili.
Beki wa kushoto: Andre Santos

Beki wa kushoto alijiunga na Arsenal mwaka 2011, aliingia kwenye mgogoro na mashibiki baada ya kubadilishana jezi na Robin van Persie wakati wa mapumnziko, alikuwa mzuri sana kwenye kushambulia lakini uwezo wake wa kukaba haukua mzuri kiasi cha kuonekana ni uchochoro. Alishindwa kuendana na kasi ya mawinga wa ligi kuu ya Uingereza.
Beki wa kati: Igors Stepanov

Alijiunga na Arsenal mwaka 2000 baada ya Tony Adam kuumia, lakini hali ilkuwa tofauti kwani alicheza mechi kumi na saba tu katika miaka minne. Takwimu zake zinaonesha jinsi gani kiwango chake hakiridhisha.
Beki wa kati: Sébastien Squillaci

Took the No 18 shirt that was previously worn by Pascal Cygan and Mikael Silvestre and was similarly ineffective. Stayed for the full three years of a generous contract, even when it was clear after one season that he had little future at the club
alichukua jezi namba 18 ambayo ilkuwa inavaliwa na Pascal Cygan na Mikael Silvestre hakuwa katika kiwango chake. Alikaa miaka mitatu bila mafanikio katika kikosi cha Wenger.
Beki wa kulia: Nelson Vivas

Alisajiliwa kwa kitita cha Euro milioni 1.6 ili kuziba pengo la Lee Dixon lakini hakuwa vizuri na Arsenal ikashindwa kupata utatuzi wa tatizo la beki wa kulia imara mpaka aliposajiliwa Lauren.
Winga wa kushoto: Amaury Bischoff

Aligharimu kiasi cha Euro laki mbili na nusu (250,000) ulikuwa ni miongoni mwa usajili wa kioja kuwahi kufanywa na Arsene Wenger. Alicheza mara nne tu tena akitokea benchi.
Kiungo: Alberto Mendez

Alisajiliwa kutoka kabu ya FC Feucht ambayo ilikuwa haichezi ligi, alicheza mechi tano tu za ligi katika miaka mitano aliyokaa Arsenal.
Kiungo: Junichi Inamoto

Arrived from Japan with a huge reputation, and expectation to match, but made virtually no impact during a year at Arsenal and was quickly moved on to Fulham
aliwasili kutoka Japan akiwa na sifa za kutosha na matarajio makubwa, lakini hali ilikuwa tofauti hakuleta athari chanya zozote kwa klabu ya Arsenal na mwisho wa siku akatimkia Fulham.
Winga wa kulia: Kaba Diawara
Alinunuliwa kutoka Bordeaux kwa Euro milioni 2.5 mwaka 1999 kwa matumaini kwamba Arsene Wenger amechukua jembe lakini hali haikuwa hivyo na hatimaye akatimkia vilabu vya Marseille, PSG,Blackburn na Westham.
Mshambuliaji: Park Chu-Young

Jezi namba tisa(9) mgongoni alisajiliwa kutoka Monaco ya Ufaransa ambayo ilkuwa tayari kumuuza mchezaji kwa Lille lakini Arsenal wakaingilia kati na kumsajili. Ingawa bado yupo Arsenal lakini amecheza dakika nane katika mechi za ligi kuu.
Mshambuliaji: Francis Jeffers
Miongoni mwa wachezaji ambao hawakuwa na wakati mzuri Arsenal kinyume na matarajio ya wengi. Anakamilisha idadi hii ya wachezaji ambao Wenger aliwasajili na hawakuonesha kiwango cha kuridhisha.
Kikosi kamili hiki hapa
No comments:
Post a Comment