Kocha
mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi
hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Flames)
itakayochezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji
walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu
Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco
(Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga)
na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Naye beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali ameondolewa katika kikosi hicho kwa vile ameshindwa kuripoti kambini.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Pemium Lager inaingia kambini kesho
(Aprili 28 mwaka huu) jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
Wakati
huo huo, Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika
raundi ya pili ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Stars
itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18
wakati ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment