
Sheryl Sandberg ni mwanamke mwenye cheo cha juu zaidi katika kampuni ya Facebook
Mwanamke anayeshikilia cheo cha 
juu zaidi katika kampuni ya Facebook, amewataka wanawake kuchukua hatua 
za kubuni mazingira ya usawa kote duniani.
Sheryl Sandberg, afisaa mkuu wa mipango katika 
Facebook, amesema kuwa wanawake, wanapaswa kushikilia nafasi muhimu 
katika biashara.
"ikiwa unatafakari kuhusu kufanya 
kitu, jiulize nini unachoweza kufanya ikiwa hauna uoga na basi 
ukifanye,'' Bi Sheryl aliambia BBC.
Sandberg ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika kampuni hiyo tangu mwaka 2012.
Mwaka jana aliandika kitabu kwa jina 'Lean In' 
ambacho kinawashauri wanawake kuhusu wanavyoweza kupiga hatua katika 
nafasi zao za kazi.
"ni muhimu sana kwamba wanawake ambao ni nusu ya
 idadi ya watu wote, waanze kushikilia vyeo  katika meza za maamuzi , 
lakini bado hatujafika hapo, '' alisema .
Alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi muhimu sana katika biashara,serikali ni pamoja na kuwa wajasiri amali
Akizungumzia baadhi ya changamoto zinazokumba 
Facebook, Sandberg alisema kuwa dunia inashuhudia mageuzi makubwa ya 
kiteknolojia ambayo yanahusisha simu ya rununu na Facebook ipo katikati 
ya mageuzi hayo
No comments:
Post a Comment