Sunday, April 6, 2014

TANZANIA YABEBA KOMBE LA DUNIA BRAZIL



Timu ya Taifa ya soka ya watoto wa mtaani imefanikiwa kutwaa kombe la dunia ambalo lilikuwa linafanyika nchini Brazil. Timu hiyo ilkuwa ikipepetana na Burundi katika fainali hiyo ambapo mpaka kipindi cha kwanza kina isha Tanzania walikuwa wanaongoza kwa jumla ya magoli mawili kwa bila. Kipindi cha pili Tanzania walifanikiwa kuongeza goli tatu lakini baadae Burundi wakapata goli la kufutia machozi, mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa Tanzania 3 na Burundi 1 na hivyo Tanzania kutawazwa mabingwa wa michuano hiyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...