Tuesday, April 8, 2014

TOP 8 YA MECHI ZA UEFA AMBAZO TIMU ZILIPINDUA MATOKEO YA MECHI ZA KWANZA



8. Barcelona vs AC Milan, 2013,  KUMI NA SITA BORA

Barcelona 4 AC Milan 0 (Barcelona won 4-2 on aggregate)

Mechi ya kwanza ilipoisha watu wengi walidhani kama Barcelona ndo wameshaaga mashindano kutokana na kiwango walichokionesha kiasi kwamba ikaonekana kama ndio mwisho wa utawala wa Barcelona. Lakini mechi ya marudiano pale Camp Nou mambo yakabadilika Barcelona wakashinda goli 4 na magoli mawili kutoka kwa Messi na kuifanya Barcelona kuwa timu ya kwanza kupindua matokeo ya tofauti ya magoli mawili bila kuwa nafaida ya goli au magoli ya ugenini.

7. Juventus vs Real Madrid, 1996  ROBO FAINALI

Juventus 2 Real Madrid 1 (Juventus won 2-1 on aggregate)

Hapa miamba miwili ilikutana na wote ndio waliokuwa wanatabiriwa kuchukua ubingwa, katika mechi ya kwanza pale Hispania kijana mdogo kwa wakati huo alimaliza mchezo kwa kufunga goli moja ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Mechi ya marudiano ilikuwa na taharuki sana, katika mechi hiyo kulikuwa na kadi za njano saba na nyekundu mbili kwa timu zote. Lakini magoli mawili kutoka kwa Alessandro Del Piero na Michele Padovano yakaipaisha Juve mpaka nusu fainali ambapo walikutana na Nantes na baadae Ajax kwenye fainali namwisho wa siku Juve wakainua ndoo.

6. Arsenal vs Porto, 2011,  KUMI NA SITA BORA

Arsenal 5 Porto 0 (Arsenal won 6-2 on aggregate)

Mechi ya kwanza Porto waliibuka na ushindi wa goli 2 kwa 1 na ikaonekana kama ndio mwisho wa Arsenal lakini mambo yalibadilika Porto walipotua kwenye dimba la Emirates, walipokea kichapo cha mbwa mwizi cha magoli 5 kwa 0 na hivyo Arsenal kufuzu hatua ya robo fainali.

5. Deportivo La Coruna vs Milan, 2004, ROBO FAINALI

Deportivo La Coruna 4 AC Milan 0 (Deportivo won 5-4 on aggregate)

AC Milan hawatasahau kamwe yaliyowatokea msimu huu wa mwaka 2004 kwani mechi ya kwanza ilionekana imeshamaliza kila kitu kwa ushindi wa magoli 4 kwa 1, lakini hadithi ikawa tofauti ikiwa na mastaa kama Nesta, Pirlo na Maldini walikuta na nguvu kazi ya  Deportivo wakakubali kipigo cha magoli 4 kwa 1 na kuondolewa mashindanoni.

4. Barcelona vs Chelsea, 2000 ROBO FAINALI

Barcelona 5 Chelsea 1 aet (Barcelona won 6-4 on aggregate)
Chelsea waliwapiga Barcelona magoli 3 kwa 1 pale Stamford Bridge ama darajani, wakiwa na imani kwamba wameshafuzu kibao kikageuka walipoenda Camp Nou. Barcelona ikiwa na wakali kama Rivaldo, Luis Figo na Pep Guardiola  walianza kwa kutangulia kufunga magoli 2 ya Rivaldo na Luis Figo lakini baadae Tore Andre Flo akaifungia Chelsea na kufanya matokeo kuwa 2 kwa 1. Dani Garcia akaingezea Barca goli la 3 na kufanya mchezo uende kwa muda wa ziada ambapo Celestin Babayaro wa Chelsea akaneshwa kadi nyekundu na Barca wakapata magoli mawili kupitia kwa Rivaldo na Patrick Kluivert na kutinga nusu fainali. 

3. Monaco vs Real Madrid, 2004, ROBO FAINALI

AS Monaco 3 Real Madrid 1 (Tie drawn 5-5, Monaco through on away goals)

Baada yaushindi wa magoli 4 kwa 2 pale Santiago Bernabeu mtanange ukaamia Ufaransa na bila ajizi Monaco ambao walikuwa wanaonekana kama timu ya kawaida tu wakashangaza wengi kwa kuwachapa Madrid 3 kwa 1 nakufanya matokeo kuwa 5 kwa 5 na Monaco kufuzu nusu fainali kwa faida ya goli la ugenini.

2. Chelsea vs Napoli, 2012, KUMI NA SITA BORA

Chelsea 4 Napoli 1 aet (Chelsea won 5-4 on aggregate)

Chelsea walipigwa 3 kwa 1 pale Italia lakini Napol walipoenda darajani Chelsea ambayo kwa muda huo ndio ilikuwa imechukuliwa na Di Matteo ambaye akarudisha jeshi la zamani kundini akiwemo Drogba, Terry na Lampard waliifunga Napoli goli 3 kwa 1 ndani ya dakika 90 na hivyo kufanya mchezo huende dakika za ziada ambapo Ivanovic ndiye aliyewainua Chelsea vitini kwa goli lake safi nahivyo Chelsea kutinga robo fainali.

1. Juventus vs Manchester United, 1999 NUSU FAINALI

Juventus 2 Manchester United 3 (United won 4-3 on aggregate)

Juve walifanikiwa kupata sare ya goli 1 kwa 1 na Juve walirudi Italia wakiwa na uhakika wa kutinga hatua ya fainali. Mechi ya marudiano Inzaghi akawainua mapema Juve kwa magoli yake mawili na kuonekana kama ni vigumu kwa Man United kusonga mbele lakini magoli ya Kean, Yorke na Andy Cole yakawapeleka Man United fainali. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...