Homa
ya tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA 2014 imezidi kupanda zaidi
nchini na Jumatano hii shughuli ya upigaji kura inafungwa rasmi.
Waimbaji waliotajwa kuwania tuzo hizo mwaka huu, wanamalizia kuwaomba
mashabiki wao wawapigie zaidi kura ili waibuke washindi.
Mashabiki
wana hamu kubwa ya kufahamu iwapo wasanii waliowapigia kura watashinda
kweli ama tuzo zitaenda kwa watu wengine. Majibu ya maswali hayo muhimu
hayawezi kupata jibu leo wala kesho, bali ni usiku wa Jumamosi, May 3, kwenye ukumbi wa Mlimani City pale tuzo hizo zitakapotolewa.
Mwaka
huu tuzo za Kili zina jumla ya vipengele 34 ambapo majina ya washiriki
yalipatikana kutokana na mchakato wa kuwapendekeza uliofanywa na
wananchi wenyewe.
Ili kupata washindi katika kila kipengele, Watanzania
wamepiga kura kukamilisha asilimia 70 za kura za wapenzi na mashabiki
wa muziki nchini na asilimia 30 za kura zitatoka kwa majaji.
Majaji
mwaka huu walikuwa ni mjumuisho wa wasimamizi/waandaji na waongoza
vipindi vya chati mbalimbali za redio pamoja na runinga, wataalam wa
muziki pamoja na wadau wa muziki nchini. Majaji walikuwa 15 ambapo 8 ni
kutoka kwenye chati za muziki za redio na runinga, wawili ni wataalam wa
muziki na wa 5 ni wadau wa muziki. Utaratibu huo uliwekwa ili
kuhakikisha kuwa wanapatikana washindi halali katika kila kipengele.
Kwa
upande washereheshaji wa tuzo hizo mwaka huu, hakuna mabadiliko sana
kwakuwa Jokate Mwegelo ametangazwa kuwa mtangazaji wa red carpet na
Millard Ayo pamoja na Sam Misago wakiwahoji wasanii na wadau wengine
kwenye social media lounge.
No comments:
Post a Comment