Timu
 21 kati ya 27 zitakazocheza Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kutafuta 
tiketi ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao tayari 
zimejulikana.
Timu
 hizo ni Abajalo SC (Dar es Salaam), AFC (Arusha), African Sports 
(Tanga), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Geita Veterans (Geita), JKT Mafinga 
(Iringa), JKT Rwamukoma (Mara), Kariakoo SC (Lindi), Kiluvya United 
(Pwani), Milambo SC (Tabora) na Mshikamano FC (Dar es Salaam).
Nyingine
 ni Mvuvumwa FC (Kigoma), Navy SC (Dar es Salaam), Njombe Mji (Njombe), 
Pachoto Shooting Stars (Mtwara), Panone FC (Kilimanjaro), Singida United
 (Singida), Tanzanite (Manyara), Town Small Boys (Ruvuma), Ujenzi FC 
(Rukwa) na Volcano (Morogoro).
Kwa upande mwingine watanzania
 watano wamefanya mtihani wa uwakala wa wachezaji wa Shirikisho la 
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambao ulifanyika jana (Aprili 3 mwaka
 huu) duniani kote.
Watahiniwa
 katika mtihani huo ambao ulikuwa na maswali kutoka FIFA na Shirikisho 
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) walikuwa Godlisten Anderson, Jesse 
Koka, Lutfi Binkleb, Rwechungura Mutahaba na Silla Yalonde.

No comments:
Post a Comment