
Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.
Watu wanne, wakiwemo maafisa 
wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari 
walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi 
katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu 
vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha 
Pangani kulikotokea mlipuko huo.
                     
Alunukuliwa akisema:"kile kilichonikuta katika 
kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na 
kutoka nje."Mtaalamu wa maswala ya usalama  jijini Nairobi, 
George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa 
wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari 
la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.
No comments:
Post a Comment