MAADHIMISHO
ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambayo kitaifa yalifanyika
katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, yameingia dosari
baada ya ofisa wa Ikulu, Rashid John Chilwangwe kufariki dunia akiwa
katika maadhimisho hayo.
Chilwangwe alipatwa na tukio hilo majira ya saa nne asubuhi, nje ya
Uwanja wa Uhuru akiwa anasubiri kuingia na maandamano yaliyokuwa
yakipita uwanjani mbele ya Rais Jakaya Kikwete, yakitokea viwanja vya
Mnazi Mmoja.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa Chilwangwe ambaye anafanya
kazi katika moja ya idara za Ikulu jijini Dar es Salaam, alianguka
ghafla na kisha kubebwa na wafanyafakazi wa Chama cha Msalaba Mwekundu
na kuhifadhiwa kwenye moja ya mahema yaliyoandaliwa uwanjani hapo kwa
ajli ya huduma za dharura.
No comments:
Post a Comment