Monday, May 5, 2014

SHEDDY CLEVER AFUNGUKA KUHUSU KUKOSA TUZO ZA KTMA



MTAYARISHAJI mkali wa ngoma ya My Number One ya Staa aliyechukua tuzo saba za Killi Music Awards Abdul Naseeb’Diamond Platinumz’amefunguka kuwa ameshindwaje kuchukua tuzo za mtayarishaji bora wa mwaka wakati ngoma aliyoitayarisha imechukua tuzo ya ngoma bora ya mwaka. 
Kupitia Account yake ya Instagram aliandika hivi.. Ndugu zangu watanzania naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru saana kwa wote walionipigia kura na ata ambae hakunipigia kura ila kwa namna moja amechangia mimi kufika hapa nilipo pia naomba niwashukuru radio na tv zoote ndani na nje ya nchi ya TANZANIA. Sasa ndugu zangu hivi nitashindwa vp kuchukua tuzo ya producer bora wa mwaka wakati nimetayarisha wimbo uliochukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka na ni wimbo ambao umemfanya Msanii @diamondplatnumz aweze kuchukua tuzo zaidi ya 5 #ktma hii inaonesha kua muziki wetu watanzania bado wanahitaji elimu ya kutosha ila sina maana mbaya hapana lakini nawashukuru sana #ktma kwa kazi waliofanya pia nawashukuru wasanii wote niliofanya nao kazi na ata wale wenye ndoto za kufanya kazi na mimi. Hongera saana @diamondplatnumz kwani muziki wetu unakua pia tusubiri tuzo za MTVBASE na Imani zitakuja nyumbani. Sina mengi ndugu zangu watanzania nawapenda saana ...

Credit to cloudsfm.co

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...