Watu watatu wanaripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Mombasa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono lilitupwa
kwenye basi katika kituo cha mabasi cha Mwembe Tayari ambao hupendwa
kutembelewa na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.
Mlipuko mwingine umetokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali.
Kamishna mkuu wa polisi Mombasa, Nelson Marwa,
amesema watu 6 wamejeruhiwa na kuwa watu waliotekeleza shambulizi hilo
walitoroka kwa Pikipiki. Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la nchini Somalia.
Aidha nchi hiyo imekuwa katika tahadhari tangu
mwezi Septemba mwaka jana ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia kituo
cha biashara cha Westgate kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu
wapatao 67.
Al Shabaab ni kundi ambalo lina uhusiano na
kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limeapa kulipiza kisasi kufuatia
Kenya kutuma majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011ambayo yameungana na
yale ya Umoja wa Afrika AMISOM.
No comments:
Post a Comment