Rais Paul Kagame ameyasema hayo mjini Kigali kwenye kikao na waandishi
wa habari.Nchi za Rwanda na Tanzania zilikabiliwa na wakati mgumu
kuanzia mwaka jana kutokana na kutofautiana kuhusu kundi la waasi wa
kihutu la FDLR linaloendesha mambo yake mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya utawala mjini Kigali.
Akijibu swali mwandishi mmoja kuhusiana na uhusiano wa nchi yake na Tanzania Rais Kagame amesema hakuna sababu yeyote inayoweza kuvunja uhusiano wa wananchi wa nchi mbili jirani, aliendelea kufafanua kuwa matatizoo yanayowakabiri wananchi wa Rwanda ndio yale yanayowakabiri wananchi wa Rwanda kwa sababu wote ni waafrika, sote ni ndugu.
No comments:
Post a Comment