MSHAMBULIAJI wa 
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, amezidi kugeuka lulu kwa timu za 
Ulaya baada ya matajiri wa Urusi, CSKA Moscow nao kuonyesha nia ya 
kumsajili katika dirisha dogo linalomalizia usajili.
 
Samatta aliyeondoka nchini mwishoni 
mwa wiki kuelekea Hispania kufanya mazungumzo na moja ya timu ya huko 
inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’, sasa amekutana na zali 
jingine nchini humo baada ya CSKA nayo kumfukuzia.
 
Mtoa habari wetu aliyekaribu na 
Samatta amelipasha MTANZANIA kuwa CSKA imeridhishwa na kiwango cha 
Samatta na inataka kumsajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwenye 
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Urusi.
“CSKA kwa sasa ipo Hispania kwa ajili ya kambi ya mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi yao. Walikuwa wanamfuatilia kwa muda mrefu hivyo wanaona hivi sasa ni muda sahihi kwao wa kumsajili,” alieleza.
 
Mbali na timu kutoka Hispania na Urusi zinazomwania, chanzo hicho 
kilieleza kuwa Samatta anatakiwa na timu nyingine za Italia na Uswisi, 
huku timu mbili kati ya hizo nne kutoka mataifa hayo zikiwa ni washiriki
 wakubwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kila mwaka.
“Watanzania wasiwe na wasiwasi, taarifa njema ya Samatta inakuja muda si mrefu na itajulikana anakwenda Urusi, Hispania, Uswisi au Italia,” alieleza.
“Kwa sasa yupo Hispania na jana alitarajia kuanza mazoezi na moja ya timu hizo, watamuangalia mara ya mwisho kabla ya mazungumzo ya pande zote kuanza kisha kufanyiwa vipimo vya afya na kusajiliwa rasmi.”
 
CSKA iliyotolewa kwenye hatua ya 
makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ikiwa na Bayern Munich, AS 
Roma na Manchester City (Kundi E), kwa sasa inashika nafasi ya pili 
katika Ligi Kuu Urusi kwa pointi 34, huku Zenit yenye pointi 41 ikiwa 
kileleni.
 
Kama Samatta atafanikiwa kujiunga na 
matajiri hao wa Urusi, anaweza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao
 na kuwafikia wachezaji wengine wa Afrika Mashariki kutoka Kenya, 
Mackdonald Mariga (wakati akiwa Inter Milan) na Victor Wanyama (wakati 
akiwa Celtic).
 
Samatta alijiunga na TP Mazembe 
akitokea Simba mwaka 2011, kwa sasa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja 
ndani ya timu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Moise Katumbi.
CREDIT: MTANZANIA

mungu amtangulie mtanzania mwenzetu
ReplyDelete