Msanii
Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amekaidi adhabu aliyopewa na
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) iliyomtaka kutoshiriki masuala ya
sanaa ndani na nje ya nchi kwa mwaka mzima.
Msanii Shilole akifanya show katika jukwaa Mbeya ambapo alikuwa akimsindikiza Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dr. John Magufuli
Shilole
amekaidi adhabu hiyo baada ya kuonekana akifanya show katika kampeni za
Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimnadi Mgombea nafasi ya urais wa chama
hicho Dk. John Magufuli wakati wapo jijini Mbeya siku kadha zilizopita.
Kipindi cha Planet Bongo kilitaka kufahamu endapo adhabu ya msanii huyo imefutwa, na kuwatafuta Baraza la Sanaa Tanzania ndipo hapo Mama Sharua ambaye yupo katika Idara ya kukuza Sanaa na Masoko alipokanusha kufutwa kwa adhabu ya msanii huyo na kusema adhabu yake ipo palepale na kama amefanya shoo amekaidi adhabu hiyo.
"Shilole anatambua wazi kuwa anaadhabu hiyo hivyo kama amefanya shoo sisi kama Basata itabidi tukae chini na kufuatilia juu ya suala hilo na tukigundua kuwa kuna ukweli sheria itachukua mkondo wake," alisema Mama Sharua.
Basata imesema kitendo alichofanya msanii huyo ni wazi kuwa ameshindwa kuheshimu adhabu iliyotolewa na hivyo lazima sheria ichukue mkondo wake kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.
Planet Bongo ilimtafuta msanii Shilole kutaka kufahamu kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo ili hali anatambua kuwa anaadhabu ambayo inamkabili ndipo hapo msanii huyo aliposema kuwa tuyaache hayo mambo kwani ni mambo ya kiserikali zaidi.
CREDIT: www.eatv.tv

No comments:
Post a Comment