CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.
Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa kushindwa kulipa madeni ya walimu
nchini.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pia ametoa muda wa miezi sita kwa
Waziri huyo na Naibu wake Philip Mulogo kutekeleza hilo agizo hilo
vinginevyo chama kitawatumia wabunge wake kuwatimua kwa nguvu.
Kwa
mujibu wa taarifa za madeni zilizokusanywa na Chama cha Walimu Tanzania
(CWT), hadi sasa walimu wanadai malimbikizo yao ya Sh bilioni 49 ambayo
hajalipwa na Serikali.
Kinana alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara jana katika wilaya za Bariadi na Busega.
Alisema CCM haiko tayari kuona walimu wakinyanyaswa wakati wana madai ya msingi.
Hivi
sasa imejengeka tabia kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa wizara ya
kuwadharau walimu na hata kuwanyanyasa huku wengine wakishusha utu na
heshima ya walimu kwa kuwatukana, alisema.
Kinana
ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa alisema kwa mawaziri
kushindwa kutatua kero za walimu, imefika wakati wahusika waondoke
wenyewe na wasipofanya hivyo chama kitawaagiza wabunge wake wawafukuze
kwa nguvu.
“Ninatoa
muda wa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wakiwamo
watendaji kuhakikisha wanalipa madeni ya walimu haraka. Haiwezeni hii ni
nchi ya watu wote wakiwamo walimu wadharauliwe na hata kunyanyaswa kwa
maneno ya matusi
“Hili
hapana CCM haiko tayari kuona walimu kila siku wakipigwa danadana
kutokana na uzembe wa watu waliokabidhiwa dhamana za kuongoza sekta ya
elimu katika nchi yetu,” alisema.
MTANZANIA
ilimtafuta Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ambaye alisema hadi sasa
madeni ya walimu yamefikia Sh bilioni 49 ambayo ni malimbikizo ya
mishahara na mapunjo.
“Kila
mara tunawaambia kuwa ni vema Serikali itafute Sh bilioni 100 katika
fungu la dharura ili iweze kulipa madeni ya walimu na iachane nao lakini
hawasikii,” alisema Oluoch.
SOURCE MTANZANIA
No comments:
Post a Comment