Mh Stepphene Wassira ameishauri halimashauri ya Mtwara pamoja na halmashauri nyingine Tanzania kuwa na utaratibu wa kuandaa bajeti kwa ajili ya zoezi la upimaji wa viwanja. Akiongea katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa wilaya Mh Wassira amesema upimaji wa viwanja utasaidia wananchi wengi kupata hati za viwanja vyao ambavyo wanavimiliki na pia hati hizo zitawasaidia kutumia kama dhamana ya kupatia mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile biashara.
No comments:
Post a Comment