DK SENGONDO MVUNGI AVAMIWA
MJUMBE
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria
wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba
usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake
Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga
maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu
hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie
fedha na Dk Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga
mapanga.
Mtoto
mkubwa wa Dk. Mvungi aitwaye Dk. Natujwa Mvungi ameeleza kuwa baada ya
watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na
kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani ambapo amepatiwa
huduma ya kwanza kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
ambapo baadaye alipelekwa kwenye wodi katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa
ajili ya matibabu.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
No comments:
Post a Comment