( tarehe 30 Julai, 2014 nilitoa msimamo wangu kuhusu Bunge la Katiba kwamba liahirishwe mpaka baada ya uchaguzi Mkuu 2015. Pia nilipendekeza maeneo ya kufanya marekebisho madogo ya katiba ya sasa. Nafurahi kwamba Bunge sasa litaahirishwa. Nafurahi pia marekebisho yatafanyika. Nasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa marekebisho hayo yanafanyika yakiwemo masuala yanayohusu uchumi wa Zanzibar kama Mafuta na Gesi na Ushirikiano wa Kimataifa. Mchakato utakapoanza upya, wajumbe wa BMK wachaguliwe na wananchi moja kwa moja na wanasiasa wenye nia ya kugombea vyeo vinavyotokana na katiba wasiwe wajumbe wa BMK ).
Nilisema haya
"Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha
PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari
vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo
wangu kuhusu mchakato wa Katiba.
Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.
Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;
i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi
ii) Kuruhusu mgombea binafsi
iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano
Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.
Kabwe Zitto, MB/MBMK"
Sasa tujiandae na marekebisho hayo na tujipange kwa Uchaguzi Mkuu

No comments:
Post a Comment