Mshambuliaji
wa kimataifa wa Argentina anayechezea klabu ya Barcelona ya nchini Hispania
amevunja rekodi ya upachikaji wa magoli iliyokuwa inashikiliwa na Paulino
Alcantara. Paulino Alcantara ambaye ni mzaliwa Philippines aliichezea Barcelona toka mwaka 1912 mpaka 1927 alifanikiwa
kufunga magoli 369 katika michezo 357 ukijumuisha ya kirafiki.
Ikumbukwe
pia miaka miwili iliyopita Messi aliivunja rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa
na Cesar Rodriguez ya upachikaji wa magoli katika mechi za mashindano, yaani
magoli ambayo hayausiani na mechi za kirafiki.
Messi
mwenye umri wa miaka 26 amevunja rekodi ya Paulino jana katika mechi ya la liga
iliyowakutanisha na Osasuna, katika mchezo huo ambao Barcelona waliibuka na
ushindi wa mabao 7 kwa bila Messi aliifunga magoli matatu na kufikisha idadi ya
magoli 371 ukijumlisha na yale ya michezo ya kirafiki.
Baada
ya kuivunja rekodi hiyo Mess kwa sasa anafukuzia kuivunja rekodi nyingine ya
upachikaji wa mabao kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, ambapo Raul Gonzalez wa Real
Madrid ndiye anayeshikilia rekodi hiyo kwa kupachika mabao 71 wakati Messi
mpaka sasa ana magoli 67.
huyu jamaa c siri 2mpeni 2 respect zake maan dah!!! yaan hapo ndio kwanza ana miaka 26
ReplyDelete