Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Gitaa Supertalent ambaye
alishawahi kusumbua na kibao chake matata sana kinachoitwa Homa ya Mapenzi hivi
karibuni anatarajia kuachia ngoma mpya ambayo imesimamiwa na mikono salama ya
mtayarishaji mkali wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo Aby Dady. Track hiyo
mpya ipo katika hatua za mwisho ya kukamilika kwa video yake ambayo itakuwa na viwango
vya kimataifa.
Kwa mujibu wa Gitaa ambaye ni mkali wa masauti jina la track
hiyo bado halijawekwa wazi ila ipo katika hatua ya mwisho kukamilika kwa hiyo
wapenzi wa mziki mzuri wakae tayari kwa mkao wa kula kwa ajili ya kupokea mziki
mzuri kutoka kwa kijana mwenye kipaji cha hali ya juu Gitaa Supertalent.
No comments:
Post a Comment