Saturday, April 23, 2016

MBAO FC YA MWANZA YAPANDA LIGI KUU BARA(VPL) BAADA YA GEITA GOLD MINES KUSHUSHWA


Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) limeitangaza rasmi timu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza kupanda ligi kuu ya Tanzania Bara(VPL). Maamuzi haya yamefikiwa baada ya kamati ya nidhamu kuzishusha timu nne kutoka kundi C ambazo zilikutwa na hatia ya kupanga matokeo. Mbao FC imeongoza kundi hilo kwa pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu nne zilizokumbwa na mkasa huo ambazo ni Geita Gold Mine, Jkt Kanembwa, JKT Oljoro na Polisi Tabora.

Wakati huo huo kamati ya rufaa ya TFF inatarajia kukutana jumamosi ya tarehe 30 ya mwezi huu wa nne kujadili rufaa zilizokatwa na baadhi ya watuhumiwa. Waliokata rufaa ni Salehe Mang'ola, Yusuph Kitambo, Amosi Mwita, Fateh Remtullah, timu ya JKT Oljoro na Polisi Tabora.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...