Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando kwenye
michezo ya mwishoni mwa juma baada ya kufanya makosa kwenye michuano ya
ligi kuu kumwondoa kimakosa mchezaji wa Arsenal wakati timu hiyo
ilipopoteza mchezo kwa kuchapwa magoli 6-0 na Chelsea.
Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku
ya Jumamosi baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kushika mpira, lakini
Kieran Gibbs aliondolewa kimakosa
Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa
kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa awali ndio ulikua
wa mwisho.
Hata hivyo baadae Mariner alikiri na kuomba
radhi kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua
aliyepaswa kuadhibiwa katika mchezo huo.
Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema
kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara
nyingi husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi
No comments:
Post a Comment