Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea amethibitisha kuungana na
rapa Snoop Dogg katika video yake mpya. Mromania huyo mwenye umri wa 35,
alihusihwa na tetesi hizi na baadae akathibitisha kupitia kwenye akaunti yake
ya Instagram.
"Coming soon!", "Stay tuned!" Mutu aliandika kwenye akaunti yake.
Akiongea na vyombo vya habari Massimo Caroletti muongozaji
ambaye huwa nafanya kazi kwa ukaribu na Snoop Dogg alisema Mutu ni mtu muhimu sana kuwepo kwenye
hii video na yupo tayari.
Mutu ambaye mwaka jana alifungiwa kuchezea kikosi cha
Romania baada ya kumfananisha kocha wake na mchekeshaji Mr Bean.
Snoop mwenyewe pia ni mtu ambaye anapenda soka na alianza
kupenda soka baada ya kuwa anacheza sana game za soka.
“nilipokuwa nacheza gemu za soka pia nilikuwa najifunza
kuhusu mchezo huo mwisho wa siku nikaanza kuangalia mechi halisi kupitia TV. Sasa
hivi naupenda sana huu mchezo”
No comments:
Post a Comment