Kikosi cha Barcelona usiku wa jana kimeuaga mwili wa aliyekuwa kocha wao, Tito Vilanova kabla ya mazishi yake.
Wachezaji
 wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu 
katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za 
mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45 
baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani.
Mkewe
 na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao 
kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota, 
alilia sana.
Heshima
 za mwisho: Kutoka kushoto, Victor Valdes, Carles Puyol, Xavi na Andres 
Iniesta wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili wa Tito Vilanova

Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia

Lionel Messi alikuwepo pia kumuaga Vilanova

Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45
Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji wa Barcelona, Lluis Martinez Sistach.
Marais
 wa zamani wakiwemo Joan Laporta na Sandro Rosell walikuwepo kanisani, 
pamoja na Wajumbe wa bodi walioongozwa na Rais wa sasa, Josep Maria 
Bartomeu.
"Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza.

 Gerardo Martino (kushoto) na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo

Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana

Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia

No comments:
Post a Comment