Wednesday, April 30, 2014

Tsvangirai amtimua hasimu wake


Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai aliyetimuliwa kutoka katika uongozi wa chama chake cha MDC amesema kuwa hasimu wake katika chama hicho Tendai Biti, naye ametimuliwa pamoja na wanachama wengine 8.
'Bwana Biti ni mtegemea tu cha wengine ambaye anatumiwa na rais Robert Mugabe,'' alisema Tsvangirai.
Mnamo siku ya Jumamosi, mrengo mmoja wa chama hicho unaoongozwa na Biti ulisema kuwaTsvangirai, alisimamishwa uongozi wa chama kwa muda, kwa sababu ya kukosa uwezo wa kuongoza chama hicho.

Mgawanyiko katika chama cha MDC, unakuja baada ya chama hicho kushindwa vibaya katika uchaguzi uliofanyika 2013.Uchaguzi huo ndio ulikuwa mwisho wa muungnao uliokuwepo kati ya chama tawala Zanu-PF na MDC ulioundwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2008 uliokumbwa na utata.

Tsvangirai na Bwana Biti, ambaye ni katibu mkuu wa chama cha MDC walikuwa washirika kwa muda mrefu katika kampeini yao dhidi ya Mugabe, ingawa walitofautiana Julai mwaka jana.
Tsvangirai alisema Biti na wanachama wenzake aliowaita waasi, wameondolewa katika vyeo vyao kama wabunge.

"alituhadaa, Mwanamume huyu hata haamini chochote isipokuwa mamlaka,'' alisema Tsvangirai kuhumusu Biti.
Mnamo siku ya Jumamosi mrengo wa bwana Biti ulisema kuwa baraza la chama cha MDC lilipiga kura kumondoa Tsvangirai kutoka katika uongozi wa chama hicho, wakisema kuwa chama hicho kimeguzwa na kuwa kama himaya ya mtu mmoja.

Kwa upande wake Tsvangirai alipuuza mkutano huo kama usio halali na ulio kinyume na katibaWafausi wengi wa MDC, wana wasiwasi kuwa malumbano hayo yanaweza kuimarisha utawala wa Mugabe na chama chake na wanatumai kuwa wataweza kusuluhisha tofauti zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...